Baadhi ya wanachama wa UVCCM Mkoa wa Kigoma wakifanya usafi katika hospital ya mkoa wa kigoma.

Mbunge wa viti maalum kupitia umoja wa vijana Zainabu Katibu akiwafariji watoto waliolazwa katika hospitali ya Mkoa wa Kigoma
Na Editha Karlo wa blog ya jamii, Kigoma
Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma(UVCCM) wamefanya usafi katika hospitali ya Mkoa wa Kigoma (Maweni) sambamba na kuwafariji wagonjwa waliolazwa katika wodi mbalimbali hospitalini hapo.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa mbunge wa viti maalum kupitia umoja wa vijana Zainabu Katimba alisema kuwa wameamua kuwafariji wagonjwa na kufanya usafi hospitalini hapo ili kuendana na kasi ya Mhe. Rais ya hapa kazi tu.
"Sisi kama vijana tumeamua kutekeleza kauli mbiu ya Mhe.Rais Magufuli ya hapa kazi tu kwa vitendo na hii si kwaajili ya siku ya uhuru tu kesho hili ni zoezi endelevu tutakuwa tunalifanya mara kwa mara"alisema Bi.Katimba
Aliwataka wananchi wote bila ya kujali itikadi zao kumuunga mkono Mhe.Rais kwa kujitokeza siku ya kesho na kufanya usafi katika maeneo yao kwani kwa kufanya hivo itawasaidia kuepukana na maradhi ya milipuko kama kipindupindu na mengine.
Naye mwenyekiti wa umoja wa vijana(UVCCM)Mkoa wa Kigoma Peter Msanjile alisema kuwa zoezi hilo la usafi katika maeneo mbalimbali linatekelezwa na vijana katika Wilaya zote.
Msanjile amempongeza Rais wa awamu ya tano Mhe.Pombe Magufuli kwa kwa kazi nzuri anayoifanya.
"Sisi tupo hapa hospital ya mkoa lakini pia na wenzetu waliopo mawilayani nao wanaendelea na zoezi hili katika maeneo mbalimbali kama masokoni,hospital na kwenye vituo vya watoto yatima"alisema mwenyekiti huyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...