Mwanzilishi wa kikundi cha Tanzania Talents Organisation, Isaya Msabila akizungumza na mwandishi wetu leo jijini Dar es Salaam katika eneo wanalofanyia mazoezi kata ya Kwembe jimbo la Kibamba. Kikundi hicho cha sanaa za maigizo na ngoma asilia hapa nchini ambapo wameungana vijana 26 ili kupunguza idadi ya vijana wasio na ajira wameona kujikusanya na kufanya maigizo na ngoma asilia ili kujikwamua kiuchumi.
Vijana wa kikundi cha maigizo na ngoma asilia cha Tanzania Talents Organisation wakiwa katika picha ya moja leo jijini Dar es Salaam.
VIJANA 26 wameunda kikundi cha maigizo na mgoma za asili kijulikanacho kama Tanzania Talents Organisation(T.T.O).Kwembe jijini Dar es Salaa ili kupunguza ongezeko la vija wasio na ajira hapa chini.
Kikundi hiki cha maigizo na ngoma asilia kilichojichimbia katika kata ya Kwembe jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam kikiwa na leongo la kutunza asili na tamaduni ya watanzania ili iweze kuigwa na mataifa mengine ulimwenguni kote.
Hayo yamesemwa na Mwanzilishi wa kikundi cha Tanzania Talents Organisation, Isaya Msabila wakati akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo.
Pia Msabila amesema katika kikundi hicho wanachangamoto kadhaa baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi pamoja na huduma ya kwanza kwa vijana hao endapo kama kukitokea majeruhi katika harakati za kuigiza au kufanya mazoezi.
Msabila aliwaomba wadau mbalimbali wanaoweza kusaidia kikundi hicho cha sanaa za uigizaji na ngoma asilia awasiliane na mwanzilishi wa T.T.O
Isaya Msabila kwa namba 0714419415 ili kuweza kukisaidia kikundi hicho kwa namna mbalimbali ili vijana waweze kujikwamua kiuchumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...