Na Jacquiline Mrisho
Maonesho ya utamaduni wa watu wa China yalifanyika jana usiku maeneo ya Makumbusho ya TaifaJijini Dar es salaam baada ya ufunguzi rasmi wa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China uliofanyika mchana.
Maonesho hayo yalifunguliwa na Mkurugenzi wa kituo hicho cha Utamaduni wa watu wa ChinaTanzania Bwana GAO Wei ambapo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wageni waalikwakuangalia utamaduni wa wachina kupitia muziki wao.
Hafla hiyo ilipambwa na wanamuziki mahiri wa kundi la watafiti wa muziki wa asili linaloitwa Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China kilichopo Beijing.
Wanamuziki hao walianza kwa kupiga vyombo vyao vya muziki kwa pamoja bila kuimbachochote na baadae kila mmoja wa wanamuziki hao alipiga chombo kimoja cha muziki ilikuwaonyesha wageni waalikwa sauti na mdundo wa kila chombo cha muziki.
Mwishoni walipiga vyombo vyao kwa pamoja kwa kupiga mapigo ya wimbo wenye asili yakitanzania unaoitwa ‘Malaika Nakupenda’.
Kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania ndio kituo cha kwanza kufunguliwa kwa Afrika Mashariki. Kimefunguliwa rasmi jana saa nne kamili asubuhi.Kituo hicho kipo Barabara ya Hassan Mwinyi maeneo ya Upanga Jijini Dar es Salaam.
Msanii wa kundi la Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China Yang
Jing akionyesha umahiri wa kutumia vifaa vya muziki wakati wa Tamasha la
Forbidden City Chamber Orchestra lililofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa
Makumbusho ya Taifa jana jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilikuwa maalumu
kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China hapa nchini
Msanii wa kundi la Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China Di Yang
akionyesha umahiri wa kutumia vifaa vya muziki wakati wa Tamasha la Forbidden
City Chamber Orchestra lililofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa Makumbusho
ya Taifa jana jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilikuwa maalumu kufuatia
kuzinduliwa rasmi kwa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China hapa nchini.
Mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa Watu wa China nchini
Tanzania Bw. Gao Wei (watano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
wanamuziki wa kundi la Zijincheng kutoka
Chuo Kikuu cha Sanaa cha China. Kundi hilo linaundwa na wanazuoni na watafiti
wa muziki wa asili nchini China.
Picha na Frank Shija, WHVUM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...