Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Philip Mpango (Kulia)akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa ya upatikanaji wa makontena 43 pamoja na malipo ya kodi ya Zaidi ya shilingi bilioni tano kutoka kwa wakwepa kodi,kushoto kwake ni kaimu Kamishna Mkuu wa TRA Bw.Lusekelo Mwaseba.
 Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Bw.Lusekelo Mwaseba(Kushoto) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Philip Mpango.
Mkurugenzi wa Huduma na elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Bw. Richard Kayombo akieleza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Philip Mpango.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)  imewasimamisha kazi wafanyakazi  35 wakiwemo 27 waliokamatwa katika geti namba tano na sasa wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano na uchunguzi.
BAADA ya Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kufanya ziara ya kushitukiza katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kubaini upotevu wa Makontena 329, Makampuni 43 yameonekana kuhusika kukwepa kodi ya Sh.Bilioni 12.6.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango amesema kuwa kampuni hizo 43 zilipitishiwa Kontena katika Bandari Kavu ya Said Salim Bakhressa na kutaka ndani ya siku sita kuanzia leo kampuni zote ziwe zimeshalipia kodi kutokana na idadi ya kontena.
Dk. Mpango amesema katika kampuni ambazo zilizokwepa kodi ambazo zilipitisha Kontena 329 wameshalipa zaidi ya Sh. Bilioni Tano(5) ambapo wanatakiwa kulipa kodi iliyobaki kuweza kumaliza kodi ya Sh.Bilioni 12.6 kwa kipindi alichoweka Rais Dk .John Pombe Magufuli. 
Amesema kuwa hatilafu za kupotea kwa makontena hayo, kazi hiyo walishakuwa wameanza kwa bahati mbaya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa Majaliwa aliwawahi wakati alipofanya ziara katika mamlaka hiyo.

Kampuni zilizokwepa Kodi ya mapato kwa makontena 329 ni Lotai Steel Tanzania LTD yenye makontena 100,Tuff Tyres Centre Company kontena 58 Binslum Tyres Company LTD, Kontena 33, Tifo Global Mart (Tanzania) Company Limited Kontena 30,IPS Roofing Campany Ltd Kontena 20,Rashywheel Tyre Center Com.Ltd Kontena 12, Kiungani Trading Company Ltd 10 Homing International Limited Kontena 9, Red East Building Kontena Saba,Tybat Trading Co Ltd, Kontena Tano,Zing Ent Ltd,Kotena Nne,Juma Kassem Abdul, Kontena Tatu, Salum Continental Co.Kontena Mbili, Zuleha Abbas Ali Kotena Mbili na Snow Leopard Building Kontena mbili na waliobaki walikuwa na kontena moja moja.

Aidha amewataka wafanyakazi kuwasilisha mali zao ili kuweza kuangalia uwezo wake katika utumishi kama zinaendana na umiliki huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Haya majizi wote hawakuanza kazi zao jana ama juzi. Nitakacho kujua mimi ni vipi tumeamka ghafla, na siku zote zilizopita mbona tulikuwa twatembea with our eyes closed.

    ReplyDelete
  2. SIO DAR TU WAENDE TANZANIA NZIMA ,MWANZA, BUKOBA, TABGA , KIGOMA,NAMANGA MUONE MIJIZA YA MAFISADI WALIVYONEEMEKA NA ULAJI WA TRA

    INATISHA HII SIO TANZANIA AFADHALI CONGO

    ReplyDelete
  3. Hii ni serikali shupavu. Tuipe ushirikiano wa kutosha ktk vita dhidi ya ufisadi na maovu mengine. Naomba MWENYEZI MUNGU aibaliki serikali hii na nchi yetu Tanzania.

    ReplyDelete
  4. HATA HAWA SINA IMANI NAO...WEZI TU

    ReplyDelete
  5. mlikuwa wapi siku zote mpaka kampuni zinakuwa nyingi?

    Na zimekwepa kwa miaka mingapi?

    Kodi ya miaka yoote ilipwe.

    ReplyDelete
  6. Ndio maana walishikia bango "kutaka mabadiliko", kumbe ulikuwa mpango wa kupata chaka kubwa zaidi la kujificha!

    Hali ingekuwa jumping from pan to fire!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...