Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel wamefanya
sherehe za kufunga mwaka zilizofanyika katika hotel ya Double Tree mwishoni mwa
wiki hii jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo pia wafanyakazi wa kampuni hiyo upande wa Zanzibar
wamefanya sherehe za kufunga mwaka katika hotel ya Zanzibar Beach Resort.
Akizungumza wakati wa sherehe hizo Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit
Janin, amewapongeza wafanyakazi wote wa Zantel kwa ubunifu na uchapakazi
waliounyesha katika kampuni hiyo.
‘Nawapongeza sana wafanyakazi wa Zantel kwa uchapakazi na
ushirikiano waliounyesha kwa mwaka huu mzima, hasa katika maeneo ya huduma kwa
wateja na ubunifu wa bidhaa mpya’ alisema Janin.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akitoa hotuba fupi ya kuzindua sherehe ya
kufunga mwaka kwa wafanyakazi wa Zantel iliyofanyika mwisho wa wiki.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Zantel, Bertrant Lacroix akijihudumia chakula wakati wa sherehe
ya kufunga mwaka ya Zantel. Anayemfatia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel,
Progress Chissenga.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Zantel akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi wakati wa
sherehe ya kufunga mwaka kwa Zantel.
Mkurugenzi
wa Rasirimali watu wa Zantel, Bi Joanita Mrengo akizungumza wakati wa sherehe
ya kufunga mwaka kwa wafanyakazi wa Zantel.
Mshauri
wa Masuala ya serikali wa Zantel kwa upande wa Zanzibar akizungumza wakati wa
sherehe ya wafanyakazi iliyofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa
Zanzibar Beach Resort.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...