WANAUSALAMA wa mtandao  duniani kote walikamilisha tukio muhimu sana linalofanyika kila mwezi Oktoba (Cybersecurity Awareness Month) lenye dhamira ya kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao huku ikiaminika kupitia tukio hilo uhalifu mtandao unaweza kupunguzwa kwa asilimia kubwa. Mataifa mengi yakiwa na mafanikio makubwa kutokana na hili ambapo Tanzania pia kupitia baadhi ya Makampuni ilipata kushiriki.

Wakati bado mafanikio mbali mbali yakijadiliwa wahalifu mtandao wamegundulika kuja na uhalifu unaotafsiriwa kuwa ni wa kihistoria na uliofanyika kwa ubunifu na umahiri wa hali ya juu ambapo wahalifu mtandao wamefanikiwa kusambaza kirusi aina ya ModPOS kinacho athiri mashine zinazotumika kukamilisha miamala wakati wa manunuzi.

Kirusi cha ModPOS, kimegundulika Nchini Marekani wakati wa sherehe za “Thanks Giving” ambapo watu wengi hufanya manunuzi. Kirusi hicho Kimekua kikifanikisha upotevu mkubwa wa pesa wakati wa miamala.
Mara baada ya ugunduzi huo wa ModPOS, mijadala kupitia mtandao ilianza baina ya wanausalama mitandao ili kuweza kufanikisha mambo makubwa matatu. Moja ni kuweza kugundua chanzo na jinsi ilivyo fanikishwa kuwepo bila kugundulika (Inaaminika kimedumu muda – Taarifa ambazo bado zinafatiliwa) Pili, Ilikua ni kutafuta suluhu ya kirusi hicho ili kiweze kuondolewa na Tatu, ni kupanga namna ya kukuza uelewa wa namna ya kujikinga na janga hili la ModPOS.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...