Na Krantz Mwantepele, Geita
Ni miaka mitatu na miezi nane toka mraghbishi Fedson Yaida na wenzake toka vijiji vya jirani kukutana na Chukua Hatua. Ni rafiki waliyekutana naye mwaka 2011 katika mazungumzo maalumu ambayo walitakiwa kuyafikisha kwa wananchi wenzao wa vijiji vya Shenda, Iponya, Nyakasumula na Bukandwe katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Ni katika mazungumzo hayo ya siku tatu, ambayo Fedson toka kijiji cha Shenda alibadilishwa na kuwa mraghbishi wa aling’amua uwezo alio nao katika kusimamia rasilimali za kijiji chao, suala ni angezisimamiaje wakati yeye si kiongozi na ni jukumu la wanakijiji wote. Katika mazungumzo hayo rafiki yao, Chukua Hatua aliwaambia, “Ni jukumu lako Fedson na waraghbishi wengine mliopo hapa, ni jukumu lenu la msingi kuj i t aj i r i sha kwa taarifa na maarifa.
Kwa kufanya hivyo mtakuwa na uwezo wa kujenga hoja mkizithibithisha na vielelezo. Hivyo ni jukumu lenu kujua ni wapi na toka kwa nani mtapata taarifa na vielelezo vya hoja yenu. Uzito wa hoja na maelezo kwa uthibitisho ni silaha muhimu kama mnataka kushawishi wenzenu kuchukua hatua.”
Ndugu Halidi Abdu toka kijiji cha Shenda chenye wakazi wapatao 2,800 katika kata ya Masumbwi wilaya ya Mbogwe mkoani Geita;akihojiwa na mtangazaji wa redio free africa william bundala almaarufu Kijukuu cha Bibi k akielezea jinsi walivyoweza kuwaadaa viongozi wao waweze kuwasomea taarifa yao ya mapato na matumizi.
Baada ya maelezo hayo walitakiwa kwenda kutembelea halmashauri ya wilaya yao, wakati huo ikiitwa Bukombe. Na baadhi ya maeneo hayo ni ofisi za Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri. Maelezo haya yalilenga katika haki ya kupata taarifa, kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba.
“Kweli mazungumzo hayo yalinijengea uwezo mkubwa sana, Chukua Hatua alinipatia muongozo na akanipangia kwenda kwa mkuu wa wilaya. Moja kwa moja nikaonana na DC nikaanza kumuhoji mambo mbalimbali kuhusu pembejeo. Ingawa majibu aliyonipa sikuridhika nayo, lakini nilishukuru kupata nafasi ya kuongea naye. Na kwa kweli tokea siku hiyo nikawa na ujasiri mkubwa sana,” Fedson Yaida akitoa ushuhuda wa siku ambayo uoga ulimtoka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...