KWAYA ya Wakorintho Wapili ya
Wilayani Mafinga mkoani Iringa inatarajia kuzindua albamu yake ya Mchepuko sio
dili kwenye tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye
ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama albamu hiyo ina nyimbo nane
ambazo zinafikisha ujumbe wa neno la
Mungu kwa jamii.Msama alizitaja nyimbo hizo ni
pamoja na Tanzania, Mchepuko sio dili, Watenda mabaya, Ee bwana, Yahwe
tunakuinua, Tuokoe baba, Dunia hii na Hana.
Aidha Msama alisema maandalizi
ya kuelekea katika tamasha hilo yanaendelea vizuri, hivyo Watanzania wanatakiwa
kujitokeza kwa wingi kuelekea tamasha hilo.Aidha Msama alisema Watanzania walichukilie tamasha hilo
kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kutupitisha katika kipindi
kigumu cha uchaguzi Mkuu ambao ulifanyika kwa amani na utulivu ingawa kulikuwa
na viashiria vya uvunjifu wa amani.
Msama alisema waimbaji wa Tanzania watakaosindikiza tamasha
hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkobe, Joshua Mlelwa, Kwaya ya
Wakorintho wapili.Wengine watakaopanda jukwaani siku hiyo ni Martha Mwaipaja,
Jesca BM, na Christopher Mwahangila,
Sifael Mwabuka sambamba na Kwaya ya Yombo KKKT.
“Tumejipanga vilivyo na tamasha la Krismasi, hivyo tujiandae
kupiga goti la kumrudishia Mungu Shukrani baada ya uchaguzi Mkuu ambao ulikuwa
na mguso wa aina yake kutoka kwa vijana walioonesha kutaka maendeleo kutoka kwa
serikali,” alisema Msama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...