Mraghbishi Kootu Tome (wa pili kushoto) akiwa na mtendaji wa kijiji Rabie Lebuna (mwenye shati la njano) na Mwenyekiti wa Kijiji, Kerry Dukonya (wa pili toka kulia). 

Na Kisuma Mapunda,Loliondo

Sasa ni dhahiri waraghbishi wanatambua majukumu na haki zao ndani ya jamii. Uelewa wao umewapa fursa ya kuchukua hatua na kusimamia kile wanachoamini kwa manufaa ya wanajamii wanaowatumikia.

Watu hawa wamekuwa mhimili muhimu wa kuleta mabadiliko katika maeneo wanayoishi. Lakini inapendeza zaidi kuona waraghbishi hao wakijawa na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wao kwa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kama ilivyo kwenye Kijiji cha Ololosokwani, kilichopo katika tarafa ya Loliondo, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha. 

Kijiji hiki kina jumla ya kaya 1,520 zinazoundwa na vitongoji vinne vya kijiji, ambavyo ni Sero, Ololosokwani, Mairowa A na B. Baadhi ya wanaounda kaya hizo ni pamoja na waraghbishi wanaofanya kazi na mradi wa Chukua Hatua, akiwamo Kootu Tomu, mama wa watoto sita kutoka kitongoji cha Mairowa. 

 
Mraghbishi Kootu Tome (kushoto) akigawa nakala za Riwaya za Chukua Hatua kwa baadhi wa wananchi wa kijiji cha Ololosokwani ikiwa kama sehemu yake ya uraghbishi. (Picha na Kisuma Mapunda)

Tomu ni mmoja wa waraghbishi wa kwanza kuanza kufanya kazi na mradi wa Chukua Hatua wakiwa na jukumu la kufuatilia ahadi za wagombea wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010. Ni katika uraghbishi huu wa kufuatilia ahadi zilizokuwa zinatolewa na wagombea, ndipo alipojifunza taratibu na kanuni za kuwa kiongozi bora.

Miaka mitano baadaye, alijitokeza katika kinyang’anyiro cha kuomba kuchaguliwa na wanachama wenzake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kura ya ndani ya maoni. Na baada ya hapo alipata fursa ya kupeperusha bendera ya chama chake na kuchaguliwa katika uchaguzi uliofanyika mwezi Disemba mwaka 2014. 
 
Mkurugenzi Mtendaji wa PALISEP, Roberth Kamakia,akielezea jambo katika mkutano uliokutanisha waraghabishi toka mikoa ya Arusha ,Simiyu na Shinyanga uliofanyika hivi karibuni .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...