Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati) akizindua Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd. Kulia ni Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric James Shigongo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba kutoka Global.
Wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa katika picha ya pamoja na Paul Makonda mara baada ya uzinduzi huo.
KAMPUNI ya Global Publishers Ltd inayochapisha magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Championi, Risasi, Amani na Ijumaa Wikienda yanayosambazwa nchi nzima, imeandaa Bahati Nasibu kwa wasomaji wa magazeti yake ambayo inaanza rasmi Ijumaa, Desemba 11, 2015.
JINSI YA KUSHIRIKI Msomaji atatakiwa kununua nakala moja au zaidi ya magazeti tajwa na kukata kuponi moja iliyomo ndani ya magazeti hayo. Atatakiwa kujaza jina lake kamili na anwani yake na kisha kuituma kwa njia ya posta au kuipeleka moja kwa moja katika ofisi za Global Publishers au kwa mawakala wake waliyopo sehemu mbalimbali nchini. Kwa wale wa mikoani, nao wanaweza kutuma moja kwa moja kwa mawakala wetu au kutuma kwetu kwa njia ya posta.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...