Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Sharjah Khayriyyah kutoka Falme za Kiaarab wanatarajia kuwafanyia Operesheni ya moyo watoto 25. Opereshini hiyo imeanza leo na itamalizika Disemba 15, mwaka huu.
Operesheni hiyo inatekelezwa na timu ya wataalamu wanane kutoka Jumuiya hiyo kwa kushirikiana na wataalamu wa Taasisi ya JKCI.
Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi amesema kambi hiyo ni ya mwisho kwa mwaka huu na mpaka sasa wameshaweka kambi sita na kufanikiwa kufanya operesheni 176. Kati ya watu hao waliofanyiwa operesheni hiyo asilimia 85. 8 ni watoto chini ya umri wa miaka 18 na wagonjwa hao ni wa Tanzania nzima .
Idadi ya wagonjwa waliopo kwenye orodha ya kusubiri matibabu ni 478 , wkati ya hao watoto ni 366 na watu wazima ni 112.
Balozi wa falme za Kiaarabu, (United Arab Emirate) nchini Tanzania, Balozi Abdullah Ibrahim Al Suwaidi akizungumza jambo na Dk Ahamed Alkamali (kwanza kushoto). Katikati ni mmoja wa maofisa wa ubalozi kutoka nchini Tanzania.
Mkuu wa Taasisi Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohammed Janabi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upasuaji wa moyo kwa watoto 25 ambao umeanza leo katika taasisi hiyo. Wengine ni maofisa kutoka Jumuiya ya Sharjah Khayriyyah.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...