Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) amesema atakaa na Watumishi katika ofisi zao ili kubaini changamoto zinazowakabili na kuzitatua.
Mhe. Kairuki alisema hayo mapema leo wakati alipokutana na Wafanyakazi wa Idara ya Uendelezaji Sera-UTUMISHI katika kikao kazi.
“ Watu wasiwe waoga katika kazi, mimi nimekuja kufanya kazi na kila kitu kina utaratibu wake” Mhe. Kairuki alisema na kusisitiza kuzingatia taratibu zilizowekwa ni jambo la msingi.
Waziri Kairuki alisema kufanya kazi kwa ubunifu na kuwashirikisha Wafanyakazi wengine ili kutoa huduma bora na haraka kwa wananchi katika ulimwengu wa sasa ni muhimu.
Mhe. Kairuki alielekeza katika mipango ni vizuri kuwa na maeneo maalum ambayo yatatoa huduma zaidi ya moja (Huduma Centre) ili kupunguza mzunguko usio lazima, na kuokoa muda kwa wananchi wanaofuata huduma hizo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) anakutana na kila Idara na Kitengo ndani ya ofisi yake ili kubaini changamoto na kuzitatua.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Idara ya Uendelezaji Sera wakiwa katika kikao kazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb), akitoa maelekezo kwa Watumishi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI mapema leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki ( Mb), kushoto, akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Mathias B. Kabunduguru. Waziri Mhe. Kairuki anatembelea kila Idara na Kitengo katika ofisi yake kubaini changamoto mbalimbali na namna ya kuzitatua.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...