Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kulia) akimkaribisha
wizarani Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga mara baada ya
kuapishwa Ikulu, jijini Dar es Salaam leo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akimkaribisha
Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, ndani ya ofisi ya
waziri huyo iliyopo Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akisaini kitabu cha wageni
kilichopo ndani ya ofisi yake, mara baada ya Waziri huyo mpya kuingia ndani ya
ofisi hiyo baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kushoto)
akimfafanulia Waziri mpya wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kulia), shughuli
mbalimbali zinazofanywa na wizara hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John
Mngodo. Tukio hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo jijini
Dar es Salaam, mara baada ya Waziri huyo kuapishwa Ikulu leo.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akijadiliana na watendaji wa wizara
hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya wizara hiyo, mara baada ya Waziri huyo
kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Wanne kushoto ni Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo,
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), John Minja, Naibu Mkuu wa Jeshi
la Polisi (D/IGP), Abdurahman Kaniki na Kamishina wa Fedha na Utawala wa Idara
ya Uhamiaji, Piniel Mgonja (hayupo pichani).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...