Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole, kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Wakimbizi nchini. 
 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole, kuhusu masuala mbalimbali ya Wakimbizi. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Kitwanga, jijini Dar es Salaam
 Chini Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wapili kushoto) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati), kuhusu masuala mbalimbali ya Wakimbizi. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Kitwanga, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke, na kushoto ni Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNHCR, Robert Tibagwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akiwasili Makao Makuu ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Kinondoni jijini Dar es Salaam na kupokewa na Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu (kushoto). Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kikazi katika ofisi hizo kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo.  Watano kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil, wanne kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, John Mngodo. 

 Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Brenda Joshua akimfafanulia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai), jinsi wanavyosajili taarifa mbalimbali za waombaji wa vitambulisho. Waziri Kitwanga alitembelea Kituo hicho cha Usajili na kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na NIDA, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil na kulia kwa Abdulwakil ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. 
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...