Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akimkaribisha Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Dkt. Lu Youqing alipofika Wizarani kwa ajili ya kumpongeza kwa kuteuliwa katika wadhifa huo mpya na pia kuzungumzia masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na China. Pembeni ni Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki. 
Balozi Lu Youqing akizungumza na Mhe. Dkt. Mahiga kuhusu mwenendo wa ushirikiano kati ya Tanzania na China ikiwemo miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanywa nchini kwa ushirikiano na China.
Balozi Mbelwa Kairuki na Bw. Thobias Makoba, Msaidizi wa Waziri wakifuatilia mazungungumzo kati ya Mhe. Dkt. Mahiga na Balozi Lu (hawapo pichani) 
Sehemu ya ujumbe kutoka Ubalozi wa China wakifuatilia mazungumzo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. The mdudu, muheshimiwa waziri hiyo ndio chance ya kuitumia na kumuomba huyo #baloziwachinaaaa ili watusaidie kutujengea BARABARA KUBWA ZA kuanzia njia 6 kwenda na 6 kuludi hilo linawezekana ni jinsi ya sisi wenyewe kuweza kuwatumia ndugu zetu hawa WACHINA ile kisawasawa pasipo na woga wala kuweweseka hao ni ndugu zetu kabisa pasipo na shaka ni sisi tu kujipanga ipasavyo ndugu zangu watanzania wezangu nayasema haya kwa uchungu mkubwa sana because hatujui jinsi ya kuwatumia hawa wachina matenda makubwa yote tuwape wao lazima tubadilike ili kuipeleka Tanzania mbele zaidi mimi inaniuma sana China ni taifa tajiri so tuamke tupige nao kazi usiku na mchana #mwenyeuchungu kama mimi basi nakuombeni tumfikishie rais wetu msikivu na mchapa kazi hiki kilio changu ndugu zangu watanzania chance ndio hii tumsaidie hata kimawazo rais wetu Magufuli sio kila kitu tumtegemee yeye tu hili ni jukumu letu sote kwa pamoja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...