Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Palestina hapa nchini, Mhe. Hazem Shabat. Tukio hilo lilifanyika Wizarani tarehe 30 Desemba, 2015.
Waziri Mahiga akizungumza na Mhe. Balozi Mteule wa Palestina nchini, Mhe. Shabat mara baada ya kupokea nakala za hati za utambulisho wake. Katika mazungumzo yao Balozi Shabat alimpongeza Waziri Mahiga kwa kuteuliwa kwenye wadhifa huo na kumuahidi ushirikiano. Pia Waziri Mahiga alimkaribisha nchini Balozi Shabat na kumuomba aendeleze mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Palestina.
Balozi Mteule Mhe. Shabat akimkabidhi Mhe. Mahiga zawadi ya picha inayoonesha Kanisa lililopo katika mji wa Jerusalem.
Picha ya pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...