Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji, Mhandisi na Mhasibu kupeleka taarifa ya maandishi kwa katibu tawala wa mkoa juu ya ubadhirifu waliofanya wa mali za umma.
Hayo ameyasema leo wakati akiongea na watumishi wa Wilaya zote kwenye kikao cha majumuisho ya ziara yake kilichofanyika katika ukumbi wa NSSF .
Alisema kuwa katika halmashauri ya Kigoma Ujijikuna ubadhirifu wa mali za umma umefanyika wa kuuza soko la Kigodeko, Jengo la Baby Come na jengo la MI Boss kwa kiasi cha shilingi milioni mia tatu badala ya milioni 800.
Alisema kuwa anawataka wajieleze kwa katibu tawala wa Mkoa kwa maandishi ni utaratibu upi wametumia kuuza mali za umma na kwavnini walikiuka agizo la mkuu wa Mkoa la kuwataka wasiuze mali hizo.
Mhe. Majaliwa alisema kuwa maelezo yao anayataka Jumamosi January 2, 2016 yawe yamekamilika na kufika ofisini kwakwe ili kama kuna ukweli hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa kwa waliohusika na ubadhilifu huo.
Akiongea na mtandao huu juu ya tuhuma hizo mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji mhandisi Boniface Nyembele alisema kuwa ni kweli mali hizo wameuza lakini kwa kufuata utaratibu.
"Utaratibu wote tulifuata kuuza malu hizo na vikao halalu vilikaa na kupitisha na mihutasari ya vikao ipi na tenda tulitangaza tika mwaka 2013 tumeuza mwaka huu mwezi wa 6"alisema Mkurugenzi, na kuongeza kuwa fedha walizopata zilitumika katika ujenzi wa mahabara na shughuli zingine.
'Kwa kuwa Waziri Mkuu ametutaka tujieleze kwa maandish ikwa katibu tawala tutafanya hivo kwani kila kitu kipo wazi"alisema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na watumishi kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Kigoma juu ya ziara yake ya kikazi Mkoani hapa.
Baadhi ya watumishi na viongozi wa mkoa wa Kigoma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majliwa katika Kikao cha Majumuisho ya ziara yake mkoani humo kwenye ukumbi wa NSSF Desemba 30, 2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na watumishi kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Kigoma juu ya ziara yake ya kikazi Mkoani hapa.
Baadhi ya watumishi na viongozi wa mkoa wa Kigoma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majliwa katika Kikao cha Majumuisho ya ziara yake mkoani humo kwenye ukumbi wa NSSF Desemba 30, 2015.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...