WAZIRI wa Habari,Utamaduni,
Michezo na Sanaa, Nape Nnauye anatarajia kumwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex
Msama, Makamu huyo wa rais alitarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo lakini kutokana na majukumu mengine ya
kikazi, hivyo tunaendelea na maandalizi ya tamasha hilo.
Msama alisema wanamshukuru Nape kukubali kuwa mgeni rasmi
katika tamasha hilo ambalo lina mlengo wa kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya
uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.“Ni nafasi yetu kama Kampuni
na Watanzania kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kipindi ambacho kilikuwa
kigumu katika maendeleo ya Tanzania, alisema Msama.
Aidha Msama alitoa wito kwa
Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo kwa sababu ya kufikisha
shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu.
Alitaja viingilio kwa VIP ni
shilingi 50,000, viti maalum shilingi 10,000, viti vya kawaida shilingi 5000 na
watoto shilingi 2000.Msama aliwataja waimbaji
watakaopanda jukwaani siku hiyo ni pamoja na Rebecca Malope (Afrika Kusini),
Solomon Mukubwa, Sarah K, Faustin Munishi (Kenya), Rose Muhando, Upendo Nkone,
Jesca BM, Joshua Mlelwa, Kwaya ya Wakorintho Wapili na KKKT Yombo.
“Maandalizi yamefanyika kwa
kiasi kikubwa yamefanyika, hivyo nawaomba Watanzania tujitokeze kwa wingi siku
hiyo ili kufanikisha asante kwa Mungu,” alisema Msama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...