Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye aliyekuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi albam mbili za kwaya ya Wakorintho wa Pili kwenye tamasha la Krismas lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo, ambapo mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini Rebecca Malope amefanya onesho kubwa lililovuta hisia za mashabiki wengi waliohudhuria katika tamasha hili akishirikiana na waimbaji mbalimbali wa hapa nyu mbani na nchi jirani ya Kenya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Nape Nnauye amewaomba watanzania kuzidi kumuombea Rais Dk . John Pombe Magufuli kwa kazi ya kutumbua majipu ambayo amekwishaianza kwani kazi hiyo ni ngumu na ina vikwazo vingi, lakini pia amewataka watanzania na waumini wa madhehebu mbalimbali kuwaombea wasaidizi wake ili waweze kuwa bega kwa bega na Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli ili kutekeleza kazi hii kwa ufanisi na kisha watanzania wafaidi matunda na rasilimali zao wenyewe.
Waimbaji kutoka Kenya walikuwa ni Faustine Munishi na Sara K na Solomon Mukubwa kutoka jiji la Nairobi huku waimbaji wa hapa nyumbani wakiwa ni Rose Muhandom Upendo Nkone, Christine Shusho, Edson Mwasabwite, Joshua Mlelwa na wengine wengi, Tamasha hilo pia lilikuwa na lengo la kumshukuru mungu kwa nchi yetu ya Tanzania kufanya uchaguzi kwa amani, Kulia ni Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo.(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWEBLOG-DAR ES SALAAM)
Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo. akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye ili kuzungumza na wananchi katika tamasha hilo kushoto ni Mbunge Martha Mlata na MC Mwakipesile mshereheshaji wa Tamasha hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...