Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu akimjulia hali mmoja wa watoto waliolazwa kwenye wadi ya Watoto, Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza ili kujionea hali ilivyo Hospitalini hapo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu akimsalimia mmoja wa mama aliyelazwa kwenye wodi ya kina mama wajawazito, Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Donan Mmbando.
Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam akisikiliza malalamiko mbalimbali toka kwa wananchi waliofika Hospitalini hapo kupatiwa matibabu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo (hawapo pichani), ambapo amewasihi kutumia lugha nzuri wakati wanapotoa huduma kwa wananchi.
Baadhi ya watumishi wa hospitali ya mwananyamala wakimsikiliza waziri wakati wa majumuisho ya ziara hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu, akiongea na wananchi wanaosubiri kuingia Hospitali ya Mwananyamala kuangalia ndugu zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Safi mama ummy kwa kuendeleza kauli ya hapakazitu

    ReplyDelete
  2. Hii timu is complete
    I like u guyz

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Mh.Ummi kwa kuamua kusiliza kero za wananchi.
    Viongozi wakiwasikiliza wananchi kwa namna hii, na pia wakiwasikiliza wafanyakazi, halafu wakatafuta suluhisho la matatizo, basi nadhani tutafanikiwa.
    Hongera serikali ya awamu ya tano,kwa yote haya....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...