Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk.Diwani Msemo ili kupisha uchunguzi pamoja na mambo mengine ili kubaini  mgongano wa kimaslahi ulioathiri utendaji wa taasisi  hiyo chini ya kaimu mkurugenzi huyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto mwenye Wizara hiyo, Ummy Mwalimu imesema kuwa kutokana na ziara alizofanya Rais Dk. John Pombe Magufuli inaonyesha kukosekana kwa dawa katika hospitali za Serikali huku vituo vya afya vya  binafsi vikiwa na dawa.

Taarifa ya Waziri huyo imesema kuwa upungufu wa dawa umeendelea kujitokeza kwa karibu zaidi na baadhi ya wagonjwa walieleza kwa uchungu jinsi wanavyopata dawa kwa tabu hatazile wanazotakiwa wapate kwa bei ya ruzuku au zilezinazotakiwa kutolewa bure na serikali.

Kwa msingi wa uwazi na uwajibikaji ameagiza watendaji wote wa sekta afya hususani wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya, Wafamasia, Wauguzi na Waganga Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya kukiri kwa maandishi kwa ngazi zao za uwajibikaji endapo wanamiliki Hospitali, Zahanati, Kiliniki, Maduka ya Dawa ndani ya siku 21 kuanzia leo Desemba 23 mwa huu ambapo  agizo hilo limeotolewa.

Aidha taarifa hiyo imedai kuwa kufanya hivyo kutaziba mianya ya upotevu wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya umma.

Bodi ya Taasisi ya Ocean Road imeagizwa kutafuta mtu atakayekaimu nafasi iliyoachwa wazi na Dk.Msemo anayefanyiwa uchunguzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. hii sio njia ya kufanya , kwa sababu mtu anaweza kuwa anamiliki duka lakini ananunua dawa zake na sio kuwa ameiba kutoka anakofanyia kazi. Njia nzuri ni kuweka muhuri ktk dawa zote za serikali ili hata zikionekana kwenye duka la binafsi zitajulikana , vinginevyo itakuwa kuwahukumu watu bila ushahidi. Mwenyezi mungu amekataza dhana kwani mara nyingi hupelekea kifikiria watu vibaya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dhana si dhambi bali hukumu bila ushahidi ni kosa.
      Hali ilivyo sasa nchini hatua hizo ni muafaka kabisa.
      Ukiona mtu ana wasiwasi jua anayo ayafichayo nayo huwa si mema, tuache nyumba isafishwe tusibiri matokeo, hatukusema mwanzo huku wengi wakiangamia na kupoteza maisha hatuna budi kukaa kimya na kuacha kupingana na utendaji unaodhamiria kuokoa maisha ya walio wengi dhidi ya walafi wachache wa mali wasiojali uhai wa binadamu wengine.
      Mungu ibariki Tanzania, Mungu wawezeshe viongozi wanaowajali waja wako!

      Delete
    2. Sawa sawa. Kheli ya wewe unalijua hilo na umenena, binadamu walio wengi huwa hawawajali wenzao kwa kuwa yeye kapata na mwenzie hana, anachoangalia ni maslahi yake tu na kumkandamiza mwenzake na kumnyonya na kumuonea hata kama ni khaki yake

      Delete
  2. Waliyonunua wanapewaga risiti waziwasilishe na rekodi za manunuzi na mauzo.

    Watakamatwa tu wezi.

    Oda yaweza tolewa waliposema wamenunua wakifoji kushusha rekodi zao pia za tarehe tajwa.

    ReplyDelete
  3. Wewe unaesema eti "hii sio njia ya kufanya", vipi hufurahishwi na hatua kama hizi. Nchi jirani wanatusifu na wengine wanatamani mazuri yanayotokea kwetu sasa yatokee pia kwao na hata Rais wetu Dr. Magufuli wanapenda awe wao na nyimbo za kumsifu kwa mazuri anayoyafanya wamemtungia. Wewe kama ni Mtanzania unatia aibu na kichefuchefu kikali sana kwa msimamo wako huo usiyo na shukurani wala kulitakia Taifa letu na wananchi wake mema. UNATUTIA AIBU WEWE KUWA MTANZANIA MWENZETU.

    ReplyDelete
  4. Ninakuunga mkono wewe uliyemjibu huyo aliyosema eti "hii sio njia ya kufanya". Na mimi ninamwambi kuwa, vitendo vya ufisadi vilivyo kithiri vya kupoteza na kuiba mapato na mali za serikali na kuzitumia kiubadhirifu, rushwa iliyo kithiri katika sector takriban zote pamoja na dhulma ya kuwanyima wananchi haki na stahili zao, vyote hivyo vinawasababishia maelfu kwa maelfu ya wananchi hali duni ya ufukara, ulemavu wa kudumu na vifo. Maharamia hao na huyo anayewaunga mkono NI WAUWAJI WABAYA SANA. Mimi kama ningekuwa Rais wa nchi yetu ya Tanzania ningekuwa nawachukulia hatua ya kuwaua kwa kuwapiga risasi hadharani kwa ajili ya kuokoa maisha ya wananchi zaidi ya 45 milioni. Vivyo hivyo kwa wale wanaowakata viungo au kuwaua Watanzania wenzetu wenye ulemavu wa ngozi na wao nao ningekuwa Rais wa nchi ningekuwa nawaua kwa kuwapiga risasi hadharani. Adhabu kali kama hii ndiyo muarubaini siyo tu wa matatizo hayo bali pia wa matatizo mengine ya mfano wa hayo "We are absolutely sick and tired of their disgusting actions".

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...