Mkurugenzi wa Huduma za mifungo Tanzania katika wizara ya Kilimo, mifugo na Uvuvi, Dkt. Abdu Hayghaimo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kusikitishwa kwao kama wizara kutokana na wanyama kuadhibiwa bila hatia yoyote kwenye migogoro kati ya wakulima na wafugaji hapa nchini. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa wizara ya kilimo, mifugo na Uvuvi, Judith Mliwa.
Daktari wa Mifugo wa kurugenzi ya huduma za mifugo wizara ya kilimo, mifugo na Uvuvi, Dkt. Christine Bukuname akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wakiwasikiliza maafisa wa wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

WIZARA ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, imekemea tabia ya kuadhibu wanyama kwenye maeneo ya migogoro baina ya wakulima na wafugaji.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za mifungo Tanzania katika wizara ya Kilimo, mifugo na Uvuvi, Dkt. Abdu Hayghaimo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Hayghaimo amesema kuwa wananchi wenye  tabia ya kuwadhuru wanyama waiache mara moja kwa kuwa wanyama hao wanaongozwa na binadamu kwenye maeneo yasiyowahusu wanayama. 

Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya ustawi wa wanyama wanahaki ya chakula, maji, mahali pazuri pakupumzika, kulindwa dhidi ya maumivu yeyote, magonjwa  na mateso ikiwa pamoja na kuwasaabishia kifo.

Pia wizara imewatahadharisha wananchi wote wanaochukua sheria  mkononi na kusababisha madhara makubwa  yasiyokubalika kutokana na migogoro ya migogoro ya wakulima na wafugaji kuwa huwanyima wanyama haki zao ni uvunjifu wa amani.

Jamii imeshauriwa kuwa itafute suruhu ya migogoro hiyo kupitia kamati zitakazo matumizi endelevuya ardhi kwa mujibu wa walaka unaoandaliwa na wizara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...