Kampuni ya simu ya Zantel leo imetangaza kuzindua ofa maalumu kwa ajili ya msimu wa  sikukuku  yenye lengo la kuwazawadia wateja wake muda wa maongezi  bure na nyongeza ya asilimia 20% katika kila manunuzi ya vifurushi au muda wa maongezi wanayofanya kupitia huduma ya Ezypesa.

Ofa hii pia itamzawadia kila mteja wa Zantel anayefanya manunuzi ya muda wa maongezi usio chini ya shillingi elfu moja kuweza kupata dakika za bure za kupiga Zantel kwenda Zantel siku za mwisho wa wiki. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Benoit Janin alisema ofa hiyo ni maalumu kwa ajili ya msimu huu wa sikukuku yenye  lengo la kukuza ubora wa  huduma na kuwapa  wateja fursa ya kufurahia huduma za mtandao huo.

“Katika msimu huu wa sikukuku tumewazawadia wateja wetu ofa hii maalumu ili iwasaidie kutumia kiasi kidogo katika kufanya mawasiliano na ndugu,jamaa na marafiki  kwenye msimu huu wa kusherekea sikukuu’ alisema Janin.Zantel kwa sasa imejikita zaidi katika kukuza na kuboresha huduma zake na kuhakikisha inaboresha maisha ya jamii ya watanzania. 

"Zantel pia imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inawafikia wateja wake na pia  kukidhi mahitaji yao ya kimawasiliano, kwa kuboresha huduma zake huku ikitoa ofa zaidi zenye kusisimua kwa mwaka 2016 'alisema Janin.



Ofa hii imezinduliwa leo, ikiwa ni wiki moja tu toka bodi ya wakurugenzi wa Zantel ilipotangaza kuzindua mtandao mpya wa 4G kwa Zanzibar pamoja na kuimarisha huduma za kimawasiliano za mtandao huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...