Mzee Balozi Paul Rupia (kulia) akizungumza katika Misa ya shukrani iliyoongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam ya Kanisa la Kianglikana Tanzania Valentino Mokiwa (kushoto) iliyofanyika katika Kanisa la St. Alban Posta Dar es Salaam jana. Misa hiyo ya shukrani ilifanyika katika kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa ambapo jana alitimiza miaka 80. Katika ni Mke wake Mama Rose Paul Rupia.
Askofu Valentino Mokiwa akitoa Baraka kwa Balozi Paul Rupia, familia yake na ndugu na jamaa waliohudhuria misa ya shukrani ya kutimiza miaka 80 ya kuzaliwa katika Kanisa Kuu la Anglikana la Mtakatifu Albano Dar es Salaam.
Balozi Paul Rupia akiwashukuru ndugu na jamaa waliohudhuria ibada ya shukrani ya kutimiza miaka 80 iliyofanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Albano Dar es Salaam jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...