JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
TAARIFA KWA UMMA
KUFUNGWA KWA MUDA BARABARA YA MPANDA - KOGA - TABORA
Tunapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa, Barabara ya Mpanda - Koga - Tabora imefungwa kwa muda kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini zilizosababisha kufurika kwa mto Koga na kufanya daraja la Koga, lililopo mpakani mwa Mikoa ya Katavi na Tabora kutopitika na hivyo kukata mawasiliano ya barabara katika mikoa hiyo.
Kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya barabara kupitia daraja hilo, tunaomba wananchi kusitisha safari kwa kutumia barabara hiyo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza hadi hapo barabara hiyo itakapofunguliwa mara tu baada ya maji kupungua katika eneo hilo.
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kifungu cha 41 (1) cha Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007 na Kanuni ya 8 (1) ya Kanuni za Usimamizi za Barabara za Mwaka 2009.
Wizara, inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki chote.
Imetolewa na:
Eng. Joseph Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI)
28/01/2016
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...