Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akizungumza na waandishi wa habari jinini Dar es Salaam leo wakati wa kuwapokea wanafunzi kumi kutoka vyuo mbalimbali ili kwenda kuwapa mafunzo na kufanya kazi katika benki hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa rasiliamali fedha wa kampuni ya Deloitte Paul Mbithi na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha utumishi wa Benki ya Barclays Tanzania, Eutropia Mwabeleko.
Mkuu wa kitengo cha utumishi wa Benki ya Barclays Tanzania, Eutropia Mwabeleko akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuwapokea wanafunzi kumi kutoka vyuo mbalimbli hapa nchini kwaajili ya kwenda kuwapa mafunzo ya kufanya kazi katika benki hiyo.
Mmoja wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Neema Munuo akiushukuru uongozi wa benki ya Barclays kwa kuwachagua kwenda kufanya kazi katika benki hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina katikati waliokaa akiwa na wanafunzi wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...