Ukimsikia mtu anapanga kwenda kumkomesha fulani kwa kumpa kipigo usitie neno lako labda kama unamzuia. Usijaribu hata kusema nenda kamfanyie amezidi. Maneno hayo ni machache lakini kisheria yatachukuliwa kama ushauri kwa mtenda kosa.
Au mtu anakwambia nakwenda kumpa vidonge vyake kwa maana ya kumtukana na kumdhalilisha na wewe unasisitiza kwa kumwambia ndio kampe maana amezidi, utakuwa nawe umeingia kwenye kosa bila kujali ulienda huko lilikotokea tukio au haukwenda . Hizi ni jinai za kila siku ambazo watu hujikuta wameingia bila kujua na wakifikishwa vituo vya polisi huanza kulaumu kuwa wameonewa kwa kuamini hawakutenda. Jihadhari. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...