WASHIRIKI wa shindano la Bongo Style linaloratibiwa na asasi isiyo ya kiserikali ya FASDO, Jocktan Cosmas Maluli  (25) na Daniel Msirikale (24) wameibuka kidedea kwa kujinyakulia tuzo za shindano hilo katika fainali iliyofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar.

Shindano hilo lililoanzishwa mtandaoni mwezi Septemba mwaka 2015, lilijumuisha washiriki wapatao mia tatu wenye vipaji vya upigaji picha na ubunifu wa mitindo huku washiriki kumi pekee wakiingia kwenye fainali baada ya michujo mbalimbali kabla ya washiriki hao wawili wakishinda tuzo hizo.

Washiriki hao walishinda kutokana na kura za majaji waliobobea katika fani hizo ambapo kwa upande wa picha majaji hao walikuwa ni: Sameer Kermalli, Hanif Abdulrasul, Idd John na Angela Kilusungu huku kwenye ubunifu wa mavazi majaji hao wakiwa ni: Martin Kadinda, Rio Paul, Zamda George na Comfort Badaru.

Jocktan Maluli ambaye ameshinda katika kipengele cha Best Fashion Designer 2015 na Daniel Msirikale aliyeshinda katika kipengele cha Best Photographer 2015, wote pamoja wamepokea kitita cha dola 500 kila mmoja huku wakipata nafasi ya kwenda nchini Ubelgiji kwa ajili ya kuonesha ubunifu wao katika maonesho ya Africa Firm Festival Belgium kuonesha kazi zao pamoja na washiriki 18 walioshiriki shindano hilo, yatakayofanyika hivi karibuni nchini humo.

Aidha washindi wa vipengele vingine ni: Shahbaaz  Yusuf aliyeshinda kipengele cha Best Personality of the Year 2015, Winfrida Touwa aliyeshinda katika kipengele cha Peoples Choice Award for Fashion Designers na Rasheed Rasheed aliyeshinda kipengele cha Peoples Choice Awards for Photograph.

Fainali hizo zilizohudhuriwa na wageni waalikwa na wadau mbalimbali wa kazi za sanaa na kupambwa na burudani mbalimbali kama vile nyimbo za asili, muziki na maonesho ya mavazi na kazi za sanaa kutoka kwa washiriki hao.

Mshindi wa Ubunifu mitindo Jocktan Cosmas Maluli A.k.a Makeke(aliyeshika cheti) akiwa katika picha ya pamoja na  waratibu wa shindano hilo kuanzia kushoto ni  Zamda George, Comfort Badaru, Martin Kadinda, Reuben Nabora na Stanley Kamana.
Mshindi wa kipengele cha The Best Photographer, Daniel Msirikale (mwenye miwani) akipokea tuzo yake.

Mlezi wa FASDO, Reuben Nabora akitoa salamu kutoka kwa mwasisi wa FASDO, Lilian Nabora aliyeko Ubelgiji.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...