Na Sultani Kipingo
Alianza na Dkt. Abdallah Possi, wakafuata Profesa James Epiphan Mdoe na Mhe. Amon Anastaz Mpanju na kusababisha mshangao wa furaha miongoni mwa wananchi wenye ulemavu kwa kile wanachokitaja kama kukumbukwa katika uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Rais alipomteua Dkt. Abdallah Possi kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu wengi walifurahi kuona Mtanzania wa kwanza mwenye ualbino anaingia katika Baraza la Mawaziri
Furaha hiyo ilizidi alipowatea Mhe. Amon Anastaz Mpanju mlemavu wa kuona kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria na Profesa James James Epiphan Mdoe kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, ambaye ni mlemavu wa miguu.
Mhe Mpanju, ambaye kitaaluma ni mwanasheria na ambaye pia alikuwa mmoja wa wajumbe wa Bunge la Katiba, alishangaza kila mtu wakati alipokula kiapo mbele ya Rais bila kusoma mahali kama ilivyo desturi.
“Huyu bwana pamoja na ulemavu wake hakika ni mtu wa kazi” alisikika mmoja wa wageni waliohudhuria hafla ya kuapishwa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu wakuu Ikulu siku ya Mwaka mpya.
Akiwa amesindikizwa na mke wake, Mhe. Mpanju alipokea Biblia Takatifu na kuinyanyua juu na kuanza kula kiapo, ingawa mkewe alikuwa ameshika karatasi ya maandiko ya vitoneambayo ilikuwa aitumie. Hata Rais alitabasamu kwa hilo.
Huko mitaani, ambako tukio hilo la kuapishwa Makatibu wakuu lilikuwa likirushwa ‘live’ na vituo kadhaa vya TV na Redio na mitandao, wengi walishikwa na butwaa, huku wakimsifia Rais Magufuli kwa kuwakumbuka watu wenye ulemavu.
Waliendelea kufurahi walipomuona Profesa James James Epiphan Mdoe, ambaye ni msomi aliyebobea katika Kemia, akisogea mbele kwa mikongojo miwili na kula kiapo cha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini.
“Tingatinga (Rais Magufuli) ametukuna kweli kwa uteuzi wa viongozi hawa”, mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Gaddy aliiambia Globu ya Jamii kwa njia ya simu kutokea mjini Iringa.
Gaddy, ambaye yeye ni mlemavu wa miguu, amesema kitendo cha kuteua wananchi wenye ulemavu kushika madarka ya juu serikalini kimewapa furaha na faraja kubwa kiasi hata yeye anajisikia ana cheo tayari.
Mwananchi mwingine wa mjini Lindi aliyesema anaitwa Mohamed Mpanyachi alipiga simu na kusema kwamba anategemea Rais Magufuli ataendelea kuwapa nafasi walemavu katika ngazi mbalimbali kwani kama walivyo hao watatu, wananchi wenye ulemavu ambao ni wasomi na wenye uwezo wa kuongoza wamejaa kila pembe nchini.
Dkt. Abdallah Possi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu - siku alipoapishwa rasmi Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 13, 2015
Profesa James James Epiphan Mdoe akila kiapo kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini mbele ya Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Amon Anastaz Mpanju akiongozwa na msaidizi wake kujiunga na viongozi wenzie ili kutia saini Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016
Kweli kabisa kilicholemaa si akili ni macho. Mungu Ibariki Tanzania na Serikali yetu na viongozi wake wote. Tuna kila sababu kujivunia nchi yetu.
ReplyDeleteI am very sorry. Huyo jamaa mwenye ulemavu wa macho anayeitwa mpanju ni mtu wa hovyo sana na mwenye kuweka itakadi za ccm mbele bila kuzingatia maslahi ya nchi.
ReplyDeleteRaisi hakupaswa kuteua mkereketwa wa ccm kwa nafasi ya naibu katibu mkuu wizara ya sheria. Haijalishi kwamba mpanju ni mlemavu. Naamini wapo walemavu wasio na makandokando ambao wanafaa zaidi kuteuliwa kwa nafasi ya naibu katibu mkuu sheria.
Naomba mufuatilie rekodi ya mpanju wakati ws bunge la katiba. Huyu mtu hafai na hupenda kutega wenzake akutafuta huruma ya ulemavu.
Uteuzi wa dr.possi nauunga mkono. Lakini ningependa awekwe wizara nyingine siyo wizara ya "walemavu." Suluhisho siyo kumteua mlemavu ashughulikie kero za walemavu wenzake.
SISI AMBAO HATUNA ULEMAVU NDIYO TUNAPASWA KUJIFUNZA NA KUBEBA JUKUMU LA KUWATUMIKIA WALEMAVU KWA WEMA,HAKI, USAWA, HESHIMA, NA UADILIFU.
Wivu tu umekujaa
DeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeletemchangiaji wa pili amesema ukweli. mpanju ni mkereketwa wa ccm kwa hiyo msitarajie akatenda haki kwa wapinzani katika nafasi aliyoteuliwa. wapinzani wataisoma namba. kaondoka dr.tulia kapachikwa mpanju.
ReplyDelete