Kampuni ya safari za ndege za bei nafuu iliyosajiliwa Tanzania, Fastjet, imezindua safari zake za Dar es Salaam-Nairobi.
Ndege ya Fastjet kutoka Dar es Salaam ilitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi na kulakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule.
Wakurugenzi wawili wa kampuni hiyo, Balozi Ami Mpungwe na Bw. Lawrence Masha, pamoja na Meneja Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Jimmy Kibati, walijumuika kwenye safari hiyo.
Kwa kuanzia, Fastjet itafanya safari za Dar es Salaam-Nairobi-Kilimanjaro na baadae itaanzisha safari za Dar es Salaam-Mombasa-Zanzibar.
Mhe. Haule alipongeza uanzishwaji wa safari hizo, akisema zitaimarisha ushirikiano kati ya Kenya na Tanzania na kukuza utalii na biashara.
Balozi Haule akiogoza kukata keki ya kusherehekea uzinduzi huo
Picha ya pamoja ya Balozi Haule na Maofisa wa Fastjet.
Abiria wakiwasili uwanja wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo
Picha ya kumbukumbu ya uzinduzi huo
Balozi Haule, Balozi Mpungwe, Bw. Masha na Bw. Kibati wakishangilia baada ya uzinduzi rasmi.akishangiliwa baada ya kukata utepe kuzindua safari za Fastje kati ya Dar es Salaam na Nairobi. Wanaoshuhudia ni Balozi Mpungwe (Kushoto) na Bw. Kibati (Kulia)







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...