Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa
Mtandao wa Thehabari.com, Joachim Mushi akitoa neno la shukrani kwa
Kampuni ya Tigo kwa kuwakutanisha baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa
mitandao ya kijamii (bloggers & website owner) katika hafla hiyo
maalumu ya chakula cha jioni iliyofanyika 'Double Tree hotel' jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wamiliki wa mitandao ya kijamii
(bloggers & website owner) wakiwa katika hafla maalumu ya chakula
cha jioni iliyoandaliwa na kampuni ya Simu ya Tigo kusherehekea mteja wa
milioni moja katika 'Facebook' ya kampuni hiyo. Tigo ilitoa zawadi
mbalimbali kwa wateja wanaofuatilia ukurasa wao (Facebook page).
Msanii maarufu wa dansi nchini, Christian Bella akiwaburudisha wageni
waalikwa katika hafla maalumu ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na
kampuni ya Simu ya Tigo kusherehekea mteja wa milioni moja katika
ukurasa wa 'Facebook' wa kampuni hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...