Jumanne tarehe 12 Januari 2016 Kituo cha Mazoezi cha Mango kilichopo Kinondoni kitaadhmisha miaka 15 tangu kuanzishwa.
Uongozi wa kituo umeandaa Bonanza la kukata na shoka ambapo wanamazoezi wote chini ya waalimu wao mahiri akiwemo Chambuso,Simba, Sukamba na Mr.Nice watashiriki katika mazoezi mbalimbali ya viungo kuanzia saa kumi na mbili asubuhi na kisha kufuatiwa na michezo mbali mbali ikiwemo ngumi, kuvuta kamba, kukimbia na gunia,kunyanyua vitu vizito na kutunisha misuli na baadaye viburudisho na muziki.
Karibuni sana wapenzi wote wa michezo mujumuike nasi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...