ISO 9001:2008
CERTIFIED
Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) ilitoa tangazo la nafasi za kazi katika magazeti mbalimbali ambapo
waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi kupitia tovuti ya TRA.
Kutokana na maombi ya nafasi
za kazi kuingiliana na shughuli za kulipa kodi mwisho wa mwezi kupitia tovuti,
TRA inasitisha kwa muda upokeaji wa maombi ya kazi kupitia tovuti hadi Jumanne Februari 2, 2016 ili
kuruhusu ulipaji wa kodi uendelee bila usumbufu.
Pia TRA imeongeza muda wa
kupokea maombi hadi tarehe 17 Februari 2016.
Waombaji wote wa nafasi za
kazi zilizotangazwa wanaombwa kutuma maombi yao kuanzia Jumanne tarehe mbili Februari 2016.
Tunaomba
radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya.
Kwa maelezo zaidi tafadhali
wasiliana na:
kituo cha huduma kwa wateja
08000780078, 0800750075,
0713800333
Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa
Mlipakodi
TRA-Makao
Makuu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...