Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu uamuzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili 


2.0 Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa

2.1 Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mahadhi Juma MAALIM ameteuliwa kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait, kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki.

2.2 Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kanda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha. Leo hii Mabalozi hao wanatakiwa kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliye chini yao. Mabalozi hao ni:

2.2.1 Bi Batilda Salha BURIANI, aliyeko Tokyo, Japan

2. 2.2 Dkt. James Alex MSEKELA, aliyeko Rome, Italia.

2.3 Rais amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Bwana Peter Allan KALLAGHE. Anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa atakapopangiwa kazi nyingine.

2.4 Kwa maana hiyo, vituo vya Ubalozi vifuatavyo viko wazi:

2.4.1 London, kufuatia kurejea nchini kwa Balozi Peter A. KALLAGHE

2.4.2 Brussels, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Deodorous KAMALA kuchaguliwa kuwa Mbunge.

2.4.3 Rome, Italia, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Dkt. James Alex MSEKELA.

2.4.4 Tokyo, Japan, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Bibi Batilda BURIANI

2.4.5 Kuala Lumpar, Malaysia, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Aziz Ponray MLIMA, kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa.

2.4.6 Brasilia, Brazil, kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Balozi, Bwana Francis MALAMBUGI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...