Na
Bashir Yakub
Kawaida serikali hutwaa
maeneo. Huhamisha wahusika wamiliki
na kuchukua eneo
kwa malengo maalum
yaliyokusudiwa. Yaweza kuchukuliwa nyumba yako, kiwanja,au hata
shamba. Mara kadhaa serikali
hufanya hivi panapo
mahitaji maalum ya shughuli
za umma kama
ujenzi wa miundombinu
kama barabara reli, huduma za umeme
na maji, ujenzi
wa shule vyuo, vituo vya
afya na miradi
mingineyo kwa manufaa
ya umma.
1.FIDIA YA
ARDHI NI NINI...
Fidia ya ardhi
ni stahili ambayo mwenye
ardhi mmiliki anatakiwa
kupata pale ambapo
ardhi yake inatwaliwa/inachukuliwa na
serikali kwa matumizi
maalum ya serikali/umma.
2. JE UNAWEZA
KUIKATALIA SERIKALI ARDHI
YAKO ISICHUKULIWE ?
Serikali
inapotaka kumhamisha mwananchi na
kuchukua ardhi yake kupisha mradi
wa umma kisheria mwananchi
hana uwezo wa
kukataa. Hii ni kwasababu
ardhi yote ni
mali ya umma
ambayo mdhamini wake
mkuu ni serikali kupitia mamlaka
ya rais.
Hivyo tunaweza
kusema kuwa ardhi
ni mali ya umma inayodhaminiwa na Serikali/Rais.
Kwa hiyo mwananchi
hawezi kuikatalia serikali kuchukua mali hiyo isipokuwa
kisheria ni kuwa
anayehamishwa apewe fidia.
Hata ukiamua kwenda
mahakamani kupinga kutwaliwa
ardhi hautapinga kuwa
serikali isichukue ardhi yako
kabisa, isipokuwa utapinga kuhusu
fidia, labda fidia
ndogo au utaratibu
mbovu uliotumika kukadiria
fidia, riba n.k.
Labda kuwe na
uonevu au hila
katika kutaka kutwaliwa
ardhi yako au namna
nyingineyo ya nia
ovu ndipo unaweza
kupinga ardhi yako
kutwaliwa. Lakini haitawezekana
kupinga hatua hiyo
ikiwa kuna malengo
maalum ya kutwaa
ardhi kwa ajili
ya shughuli za
umma. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...