MAKAMU wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu, leo Januari 5, 2016 amezindua miradi ya maendeleo katika mkoa wa Geita iliyofadhiliwa na mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania.

Mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Tshs 12Billion uliojengwa kwa ushirikiano kati ya Mgodi na serikali ambao utapunguza tatizo la maji safi na salama kwa mkoa wa Geita kwa zaidi ya asilimia 35% umezinduliwa, ambapo kwa mara ya kwanza, wananchi wa Geita wataweza kunywa maji safi na salama kutoka Ziwa Zictoria.

Tatizo la maji lilikuwa ni kero kubwa kwa wakazi wa Geita kwa miaka mingi ambapo kina mama na watoto wa kike wamekuwa ndio wakiathirika wakubwa kwa kutembea umbali mrefu ili kupata maji safi kwa matumizi ya nyumbani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makamu wa Rais alisema “Serikali ya awamu ya tano imekusudia kuleta maendeleo ya kasi kwa Wananchi kwa kushirikiana na wadau mablimbali wa maendeleo kama inavyodhihirika katika mradi huu”

Makamu wa Rais aliweza pia kutembelea na kuzindua muendelezo wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita ambayo ilijengwa mwaka 1957. GGM imeweza kutoa ufadhili wa ukarabati wa majengo hayo kwa thamani ya zaidi ya shilingi 800 Milioni ambapo ukarabati umekwenda sambamba na utoaji wa vifaa adimu kwa ajili ya vipimo na matibabu ya moyo, meno nk. Hospitali hii teule inahudumia zaidi ya wagonjwa milioni 1.7 kwa mwezi.

“Ni kusudio la GGM kuona kuwa jamii inayotuzunguka inakuwa katika hali nzuri na bora kuliko hapo mwanzo kwa kuwepo kwetu hapa Tanzania. Hii ni sehemu ya kutimiza dhamira yetu hii na tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake thabiti na kwa kuweka mazingira mazuri ya utendaji” alisema Mkurugenzi Mkuu wa GGM, Terry Mulpeter.

Miradi mingine aliyoweza kutembelea na kuzindua ni mradi wa ushonaji na kutarizi ulio chini ya mradi mkubwa wa kuendeleza uchumi kwa Wananchi wa Geita uitwao Geita Economic Development Program (GEDP) ambao unahusisha miradi ya kilimo cha Mpunga na Alizeti, Kufyatua Matofali ya Interlocking blocks na Uchomeleaji utakaoweza kuleta ajira zaidi ya 300 kwa vijana wa mkoa wa Geita.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea moja vifaa tiba vilivyokabidhiwa hospitalini hapo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM), Terry Mulpeter, ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa jamii ya watu wa Geita, leo Januari 5, 2016. wengine pichani toka kulia ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mh. Suleiman Jaffo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mh. Fatma Mwassa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita, Dkt. Joseph Kisala, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Mganga Mfawidhi wa Hospitali teule ya Mkoa wa Geita, Dkt. Adam Sijaona.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, GEITA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM), Terry Mulpeter, tuzo ya maalum ya kutambua Mchango wa Kampuni hiyo, kwa kujitoa kwake kuisaidia jamii ya watu wa Geita.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimtishwa ndoo ya maji, Bi. Tatu Salum, Mkazi wa kijiji cha Nyankubi Mkoani Geita, mara baada ya kuuzindua mradi mkubwa wa Maji Mkoani humo leo. Nyuma yake ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mh. Gerson Lwenge.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...