Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mganga Mfawidhi wa Hospitali teule ya Mkoa wa Geita, Dkt. Adam Sijaona, wakati alipofanya ziara kwenye wadi ya wagonjwa wa upasuaji ya wanaume, katika Hospitali hiyo iliyojengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM).
PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, GEITA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasalimia baadhi ya wananchi wa Mji wa Geita waliokuwepo Hospitalini hapo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (kulia) wakati wa ziara yake katika Hospitali teule ya Mkoa wa Geita, leo Januari 5, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mh. Fatma Mwassa pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Geita Mjini, Mh. Vicky Kamata.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi pamoja na wauguzi wa Hospitali teule ya Mkoa wa Geita.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea moja vifaa tiba vilivyokabidhiwa hospitalini hapo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM), Terry Mulpeter, ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa jamii ya watu wa Geita, leo Januari 5, 2016. wengine pichani toka kulia ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mh. Suleiman Jaffo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mh. Fatma Mwassa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita, Dkt. Joseph Kisala, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Mganga Mfawidhi wa Hospitali teule ya Mkoa wa Geita, Dkt. Adam Sijaona.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...