WANANCHI wa mikoa mbalimbali
wamejitokeza kuiomba kkampuni ya Msama Promotions ianzie Tamasha la
Pasaka mikoa kwao mwaka huu huku wakazi wa dare s salaam wakisisitiza
libaki mkoani humo.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama ameliambia Gazeti hili kuwa,
tayari amepokea maombi toka kwa wananchi na mashabiki wa mikoa ya
Morogoro, Mwanza, Mbeya, Dodoma na Dar es Salaam wakitaka tamasha hilo
lianzie kwao mwaka huu.
“Kamati yangu inafuata taratibu
za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambazo ni pamoja na kupata kibali
cha kufanikisha kufanyika kwa Tamasha hilo linaloshirikisha waimbaji
mbalimbali wa muziki wa Injili wa ndani na nje ya Tanzania,” amesema
Msama.
Salum Ismail Hamad ambaye ni mdau
mkubwa wa Tamasha la Pasaka amesema anawaomba waandaaaji wa Tamasha
hilo kutoliondoa jijini Dar es Salaam kwa sababu ni mkoa unaohusisha
idadi kubwa ya mashabiki wa muziki wa Injili.
Rukia Joseph wa Kimara Dar es
Salaam, alisema yeye anawapigia magoti waandaaji kutoliondoa tamasha
hilo jijini Dar es Salaam hasaa kwa waimbaji wa nje ya Tanzania kama
Solly Mahlangu na wengineo toka nje ya nchi.
Michael Deogratius alisema ni
ngependa Tamasha la Pasaka lihamie mikoani kwa sababu ya ukubwa na
umuhimu wa tamasha hilo ambalo linatimiza miaka 16 tangu kuasisiwa
kwake.Msama alisema bado wanasubiri
taratibu za kufanikisha tamasha hilo kutoka Basata, hivyo nawaomba
wakazi wa mikoani kuvuta subira wakati wakijiandaa.
Peleka tamasha la Pasaka 2016 mkoani TABORA.
ReplyDelete