Mtu mmoja Jijini Mbeya (PICHANI JUU) ambaye hakuweza kutambulika kwa
Majina,inadaiwa amekutwa amefariki leo asubuhi kwenye moja ya uchochoro wa nyumba zilizopo katika mtaa wa Mwamfupe.
Kifo cha Mtu huyo ambaye inaelezwa ni kijana wa makamo alikutwa amefariki kwenye uchochoro wa nymba hiyo mara baada ya kubainika na baadhi ya Wananchi,waliokuwa wakikatiza mtaa huo kuelekea mtaa mwingine,Baadhi ya Mashudhua wa eneo hilo wameeleza kuwa mtu huyo si mkazi wa mtaa huo,
"Mtu huyo si Mkazi wa Eneo hili, bali Jioni ya jana waliomuona maeneno hayo akiwa katika hali ya
kupepesuka Pepesuka kotokana na kunywa Pombe, na huenda hicho ndicho
kilicho pelekea Kifo chake kwani hakuwa mwenye afya njema." Alibainisha mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo wakati akihojiwa na Mwandishi wa Globu ya Jamii iliofika eneo la tukio
Baadhi ya Wanachi wa Mtaa wa Mwamfupe wakijadiliana jambo
katika eneo la tukio.
Huzuni ikatawa Eneo hilo.
Baadhi ya Wanachi sambamba na Wenyenyumba zilizo zunguka Eneo hilo la
Tukio wakisubiri msaada kutoka Jeshi la Polisi.Globu ya Jamii inafuatilia taarifa kamili kutoka kwa jeshi la Polisi mkoani Mbeya.
\Picha na Fadhiri Atick - Mr.Pengo wa Globu ya Jamii-Mbeya.
Sio wote wanaopepesuka wamelewa pengine kaleweshwa au kupewa kitu cha sumu na kushushwa hapo wafanye uchunguzi au Pengine ni kweli kalewa. Mwenyezimungu awape familia yake moyo wa subra kwenye wakati mgumu Kama huo na imani.
ReplyDelete