Na Dkt. N. T. Jiwaji,
ntjiwaji at yahoo dot com
Katika siku zijazo kuanzia sasa hadi tarehe 7 Februari Mwezi utakuwa jirani na Sayari tanzo tunazoweza kuziona kwa macho moja kwa moja.
Mwezi upo jirani na Mustarii (Jupiter) leo usiku hadi alfajiri. Baada ya siku chache alfajiri ya Februari 1 na 2 alfajiri Mwezi utakuwa jirani na Mirhi (Mars) na Februrari 3 na 4 utakuwa jirani na Zohali (Saturn) na mwisha siku za Februrari 6 na 7 alfajiri Mwezi utakuwa jirani na Zuhura na Zebaki jirani na upeo wa mashariki kabla ya Jua kuchomoza. (Angalia picha ya anga ya alfajiri iliyoambtishwa)
Tumia nafasi hii kuweza kutambua Sayari mbali mbali zitakapokuwa jirani na Mwezi siku chache zijazo wakati wa alfajiri. Fuata picha iliyambatishwa kurahisisha utambulizi wa sayari za Musharii (Jupiter), Mirihi (Mars), Zohali (Saturn), Zuhura (Venus) na Zebaki (Mercury). Mustarii na Zuhura zinan'gaa kuwa uangavu mkali kwa hiyo hutakosa kuzitambua. Sayari hutaofautiana na nyota za kawaida kwa kutofautiana kun'gaa kwa vile Sayari hun'gaa bila kumeremeta wakati nyota humeremeta.
Utatambua kua Sayari zote zimejipanga angani kwa mstari mmoja. Na hata Mwezi husogea angani kwa kufuata msatari huo. Hii inwashangaza watu lakini inelezeka kwa kuelewa kwamba Sayari zote na Mwezi zipo katika bapa moja nyembaba ambayo huunda Mfumo wa Jua. Kwa hiyo kwa wakati unaziangalia Sayari na Mwezi kutoka hapa kwetu Duniani, bapa hiyo ya Mfumo wa Jua umejiweka wima anagani na Sayari na Mwezi zipo katika bapa hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...