
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Bw. Jordan Rugimbana kwa niaba ya Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto amezindua rasmi kampeni ya kitaifa ya
uhamasishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii ( CHF) katika kata ya Nyangamara
iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini.
Katika
uzinduzi huo ulioratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Lindi Vijijini kaya zipatazo 261(sawa na
wanufaika 1,566) zilisajiliwa papo hapo katika CHF kwa mchango wa
Shilingi 10,000 kwa mwaka. Pia Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Nawanda
alihamasisha viongozi mbalimbali wa Mkoa huo ambao hawakuwepo ambapo
zilichangwa fedha kwa ajili ya kaya 2,060 za watu wasio na uwezo ili
waandikishwe katika CHF.
Katika
uchangiaji huo Mh. Waziri Mkuu ambaye ni Mbunge wa Ruangwa alichangia
usajili wa kaya 900 ambapo Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh. Rugimbana
alichangia kaya 100, RAS Lindi - kaya 100, DC Lindi - kaya 50, NHIF kaya
300, Mh. Waziri wa Habari na Mbunge wa Mtama - kaya 300, Mh. Lalinda
Mbunge wa Viti maalum CUF - kaya 50, Mh. Hamida viti maalum CCM - kaya
60, Mh. Hamid Bohali Mbunge wa Mchinga - kaya 100, Mh. Kaunje Mbunge wa
Lindi - kaya 100.

Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi akikabidhi kadi ya CHF kwa mnufaika mpya wa CHF Bw. Hassan Namangaya wakati wa Uzinduzi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa CHF Bw. E. Mikongoti alisema mkoa wa LIndi
una wanufaika 89,836 wa CHF ambayo ni asilimia 6.6 ya wana Lindi.
Alihimiza Mkoa kuifanya CHF kuwa agenda katika utekelezaji mkoani hapo
lakini pia kutumia vema fedha za uchangiaji ili kuboresha huduma za afya
ili kuvutia wengi zaidi kujiunga na Mfuko huo.
Wakati
akiwasilisha ripoti ya CHF mkoa wa Lindi, Mganga Mkuu wa mkoa Dk. Sonda
alisema Lindi imefanikiwa kupata malipo ya Tele kwa Tele ya CHF ya
SHilingi 109,436,000 kwa mwaka 2015 ambazo ni mchangi mkubwa katika
kuboresha afya mkoani humo. Hata hivyo aligusia kusema bado wana
changamoto ya hamasa ya watendaji kuhusu CHF.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...