Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Profesa Makame Mbarawa
akipokea taarifa ya Utendaji kutoka kwa Mkurugenzi wa Biashara na Maendeleo wa
kitengo cha huduma ya Makontena Bandarini (TICTS) Bw.Donald Talawa mara
alipofanya ziara ya kukagua utendaji wa kitengo hicho Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Profesa Makame Mbarawa
akitoa maelekezo kwa Viongozi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) na TICTS ambapo
amehimiza kuhusu hutoaji wa huduma kwa haraka ili kuongeza ukusanyaji wa
mapato,Kulia ni Hebel Mhanga na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bwana
Aloyce Matei.
Mtaalamu wa Uratibu wa huduma za upakuaji wa TICTS akitoa maelezo kwa
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Mbarawa (Wa tatu kushoto) jinsi ya
mfumo wa kupokea na kupakua Makontena unavyfanya kazi.
Wafanyakazi wa TICTS wakiendelea na utekelezaji wa majukumu yao ya
kupokea na kuruhusu makontena.


Viongozi wa vitengo vya bandari wamulikwe zaidi. Huchelewesha kutoa mizigo maksudi ili mteja atoe fedha za ziada. Kwa nini kutoa mzigo zisiwe siku 2 tu? Watu wengi wataitumia bandari na serikali itakusanya kodi nyingi zaidi na kujaza mabilioni kwa miradi ya maendeleo.
ReplyDeleteMoja ya mikataba mibovu kupita maelezo, ukijawa na harufu ya uvundo wa ufisadi, ni mkataba kati ya serikali na TICTS. AIBU! Inasemekana kwamba nchi nyingi duniani huwa hazibinafsishi kitengo cha upakuaji makontena bandarini kwani ndicho chenye mapato makubwa na ni rahisi kukisimamia na kukiendesha! Huwa najiuliza hivi mikataba ya aibu kwa taifa ambayo tuliingia wakati wa Mkapa hamna clause inayoipa serikali kurudi mezani ili kuirekebisha kwa maslaji ya taifa!?
ReplyDeleteWakati nikifurajishwa na kasi ya Magufuli nasubiri kuona atachukua hatua gani kurekebisha mikataba mibovu ambayo ikirekebishwa ni uhakika baada ya miaka michache tu hatutohitaji misaada vitanzi toka ughaibuni. Kwa maoni yangu, wala Magufuli hahitaji kututangazia bali anaifanya kimya kimya kwa kuwaita na kuwapa terms mpya, serikali inamiliki 50-70%, wawekezaji wa nje wanapata 0.001-45%, wakiwa wa ndani wanafika mpaka 55%.
Alafu kwenye ardhi hamna kutoa lease zaidi ya miaka 25 (renewable) kwa wawekezaji wa nje. Kwa sasa wapo wenye lease za mpaka miaka 99!
Naamini Magufuli anawavutia kasi, muda utafika! Mungu ampe ujasiri na AMLINDE ili aweze kutenda bila woga! Nawasilisha