Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Mhe Eng Godwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha Bunge la 11linaloendelea Mjini Dodoma. picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

 
Serikali imeahidi kuendelea na ujenzi wa barabara katika maeneo tofauti nchini kwa kiwango cha lami ili kutatua adha kubwa ya ubovu wa barabara ulipo katika maeneo mengi nchini.
 
Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Eng Godwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge waliouliza kuhusu mpango wa serikali kuboresha barabara zilizopo na kujenga mpya ili kukabiliana na adha ya ubovu wa barabara nchini.
 
Akijibu swali la Mhe Richard Mganga Ndassa Mbunge wa Sumve (CCM) lililohitaji  ufafanuzi wa serikali ni lini ujenzi wa barabara ya Magu-Bukwimba –Ngudu-Hungumalwa itajengwa kwa kiwango cha lami, Mhe Eng Godwin Ngonyani amesema katika  mwaka wa fedha 2014/15 na 2015/16 serikali ilitenga jumla ya shilling millioni 200 kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 70 na taratibu za kumtafuta Mhandisi Mshauri zinaendelea na baada ya kukamilika kwa usanifu na kupata gharama za mradi huo, Serikali itatafuta fedha za kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
 
Aidha akijibu pia swali la Mhe Fredy Atupele Mwakibete  Mbunge wa Busokelo (CCM) aliyehitaji kujua ni lini barabara ya Katumba-Mbambo-Tukuyu yenye urefu wa Kilometa 82 inayoanzia Katumba(RDC) kupitia Mpombo,Kandete,Isange,Lwanga, Mbambo (BDC) hadi Tukuyu (RDC) itajengwa kwa kiwango cha lami.
 
Akijibu swali hilo, Mhe. Eng Godwin Ngonyani amesema kuwa Serikali kupitia  Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, katika mwaka wa fedha 2009//10 Serikali ilianza maandalizi ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami na ambapo upembuzi yakinifu na sanifu wa kina ulikamilika na baadae Serikali iliamua kujenga kilometa 10 ambapo mwezi April,2014 Wakala wa Barabara na kampuni ya CICO ilijenga barabara hiyo kuanzia Lupaso hadi Buseji,Wilayani Busokelo.
 
Serikali kupiti Wakala wa Barabara (TANROADS) inaendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwangocha lami katika Kata, Wilaya na Mikoa mbalimbali nchini  ili kukabiliana na adha ya ubovu wa barabara ambao umesababisha watu kukosa mawasiliano baina ya maeneo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. SASA MBONA BARA BARA YA KIGOMA MPKA MWAZNZA MBONA IMEKUWA KITENDA WILI? TANZANIA YOTE INA JENGWA YAANI KIGOMA TU NDIO INA NUKSI NA SEWEKALI ZOTE KUANZIA NYERERE, MWINYI,MKAPA,KIKWETE NA SASA MAGUFULI ) HIVI KIGOMA ILIIKOSEA NINI TANZANIA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...