Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Serikali ilivyojipanga kuboresha na kuhudumia sekta mbalimbali nchini ikiwemo elimu, umeme, maji na miundombinu. Kulia ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alfayo Kidata na kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu akisistiza wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu mapato na matumizi ya Serikali yalivyoboreshwa na uchumi wa nchi kuimarika na kutengemaa.
Serikali imetoa jumla ya Sh. Bilioni 318.406 kwa mwezi wa Januari mwaka 2016, kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini na Sh. Bilioni 538.5 kwa mishahara ya watumishi wa Umma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa Serikali inajivunia kufanikiwa kutumia fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo hadi sasa Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bilioni 71.2 tu kutoka fedha za nje.
Dkt. Likwelile alisema mapato yanayokusanywa nchini yamewezesha kutekeleza sera ya elimu bure ambapo mwezi Desemba mwaka 2015 Serikali ilitoa kiasi cha Sh. Bilioni 18.77 kwa shule za msingi na sekondari kwa ajili ya ruzuku, ada na chakula kwa shule za bweni pamoja na mahitaji mengine ambapo mwezi wa Januari 2016 Serikali imetoa kiasi cha Sh. Bilioni 18.77 kwa ajili ya kutekeleza Sera hiyo.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Tunaipongeza serikali. Kwanza tunafurahishwa kuona kwenye taarifa kama hizi mpo viongozi wa juu wa taasisi na vitengo mbalimbali. Hongera sana. Pili tunaomba wafanya biashara waone fahari ya kulipa kodi. Wananchi wote tulipe kodi. Miradi ya maendeleo ikikamilika kwa wakati na uchumi kuimarika faida itarudi kwa wafanya biashara. Watu wengi watafikiwa na maendeleo hivyo biashara itapanuka zaidi. Wafanya biashara unganisheni mitaji na kuanzisha makampuni makubwa mtapata tenda serikalini. Mnapofanya ujanja mnashindwa kufanikiwa. Lakini mkifuata sheria mambo yenu yatakuwa safi. Kama serikali imeweza kulipa mishahara na kutuma ela za maendeleo maeneo husika basi hilo ni jambo la heri. Waandishi wa habari msaidie kuwaelimisha, kuwahamasisha na kuwatia moyo ili walipe kodi. Kodi yao ni manufaa yao. Serikali inapokuwa na ewezo wa kifedha hata imani ya wafanya biashara inakua zaidi. Ndio maana watu hupenda kuwekeza kwenye maeneo ya usalama zaidi. Serikali itakuwa na uwezo wa kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi. Nchi ikiwa salama, ulinzi ukiwepo biashara itakua sana na kupokea. Ushauri kwa serikali. Tusifukuze wageni. Tuwe kama Marekani. Wenye vipaji tuwafanye watumike kujenga uwezo wa nchi na kuzalisha. Mbona Marekani wanasaka watu wenye vipaji toka nchi nyingine na kuwasomesha? Hii sera ni nzuri. Wao kama wapo tuwaingize kwenye mfumo rasmi.
ReplyDelete