JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA -
TAMISEMI
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.
George Boniface Simbachawene (Mb) kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha
2(2) cha Amri ya kuanzisha Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), (The
Executive Agencies) (The Dar Rapid
Transit Agency) (Establishment) Order ) Tangazo la Serikali namba 120 la 2007, amemteua Mhandisi Ronald
Lwakatare kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu
wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es salaam (DART) kuanzia tarehe
04/01/2016.
Uteuzi
huo unafuatia kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu Bibi Asteria L. Mlambo tarehe
23/12/2015. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Ronald Lwakatare alikuwa Naibu
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road
Fund Board) akishughulikia Ufuatiliaji na Tathmini. Mhandisi Lwakatare
anatakiwa kuripoti na kuanza kazi mara moja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...