JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA,
MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAMKO KUHUSU MWENENDO WA
UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI
WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 25 JANUARI 2016
Ndugu Waandishi wa
Habari,
Wizara yangu
inaendelea kutoa taarifa ya wiki kwa umma kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa
kipindupindu hapa nchini. Hadi kufikia tarehe 24 Januari 2016, jumla ya watu 14,608 wameugua ugonjwa huo, na kati yao watu 228 wamepoteza maisha kwa ugonjwa huu. Njombe, Ruvuma na Mtwara ndiyo Mikoa
pekee ambayo haijawahi kuripoti mgonjwa yoyote wa kipindupindu, tangu mlipuko
huu uanze mnamo mwezi Agosti mwaka huu.
Kwa mujibu wa Takwimu
za kuanzia tarehe 18 hadi 24 Januari 2016, ni kuwa jumla ya Mikoa ambayo
imeripoti kuwa na wagonjwa ni 15 ambapo
idadi ya wagonjwa 524 na vifo 10 vimeripotiwa. Idadi ya wagonjwa
walioripotiwa wiki hii imepungua ukiliinganisha na idadi ya wiki iliyoishia
tarehe 17 ambapo kulikuwa na wagonjwa 621
na vifo 14 ambalo ni punguzo la
asilimia (16%). Mkoa wa Morogoro bado umeendelea kuripoti idadi kubwa zaidi
ya wagonjwa ukilinganishwa na Mikoa mingine, (Manispaa ya Morogoro 89,
Halmashauri ya Morogoro 36, Mvomero 17), ukifuatiwa na mikoa ya Mwanza (Ukerewe 36, Nyamagana 19 na
Ilemela 13), Simiyu (Bariadi DC 29
na Bariadi municipal 23), Manyara
(Simanjiro 48), Mara (Musoma Manispaa
11, Musoma DC 8, Rorya 8 na Butiama 8), Geita
(Geita DC 21 na Geita TC 6) na Mbeya (Kyela 26).
Mikoa mingine ambayo
bado pia imeendelea kuripoti wagonjwa ni pamoja na Dodoma
(Wagonjwa 22), Arusha (21), Tabora (18), Singida (18), Lindi (12), Rukwa (7),
Kilimanjaro (6) na Kagera (2).
Ndugu Waandishi wa
Habari,
Mwanzoni
mwa mwezi Januari mwaka huu, Wizara yangu kwa kushirikiana na wadau ilituma
timu ya jopo la wataalam kutoka ngazi ya Taifa kwenda kusaidiana na wataalam
waliopo katika ngazi ya mkoa na halmashauri katika mikoa 7 iliyokuwa inatoa
taarifa ya kuwa na wagonjwa wengi zaidi.
Mikoa hiyo ni Arusha, Manyara, Mwanza, Simiyu, Singida, Mara na Morogoro.
Mafanikio ya kazi iliyofanywa na Jopo hilo
yameanza kuonekana kwani katika Mikoa hiyo saba idadi ya wagonjwa wa
kipindupindu imeanza kupungua. Pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto ambazo
timu hizo ilizibaini kuwepo ambazo zinachangia kulegalega kwa juhudi za
kupambana na Kipindupindu nazo ni;
- Kuwepo na idadi ndogo ya kaya ambazo zinamiliki na kutumia vyoo bora hususani katika maeneo ambayo yameathirika zaidi na ugonjwa huu.
- Kutokuwepo kwa miundombinu stahiki ikiwemo vyoo na maji katika Maeneo ya mikusanyiko kama masoko na minada kutokuwa na
- Wananchi kutokutii sheria zilizopo kwa kuendelea kuuza chakula bila kuzingatia kanuni za afya na kuuza matunda yaliyokwisha katwakatwa maeneo yasiyo salama.
- Utiririshaji wa maji taka kwenye vyanzo vya maji, pamoja na kujisaidia maeneo ya wazi na pembezoni karibu na vyanzo vya maji.
- Kuwepo kwa idadi ndogo ya watu wanaopata maji safi na salama ya kunywa. Aidha utakasaji wa maji katika ngazi ya kaya kwa kuyachemsha au kwa kutumia vidonge vya kutakasia bado ni changamoto kubwa.
- Wagonjwa wa Kipindupindu kuchelewa kufika Kambi za Matibabu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...