
Mwanaharakati
wa mabalozi wa usalama barabarani na ASASI YA
WAZALENDO NA MAENDELEO TANZANIA Bw. Ally Nurdini Six anasikitika kutangaza kifo
cha Baba yake mzazi marehemu mzee Hassan Nurdin (R.I.P) aliyefariki
majira ya saa 9.00 alasiri siku ya Ijumaa tarehe 08 Januari, 2016 mjini Moshi.
Habari
ziwafikie ndugu, jamaa, marafiki na majirani popote pale walipo.
Marehem
Mzee Hassan Nurdin alikuwa ameugua kwa muda wa miezi sita, ambapo mtoto wake
mkubwa Bw. Ally Nurdin Six alichukua likizo kuungana na familia mjini Moshi kwa
ajili ya kumuuguza mzazi wake. Lakini Mwenyezi Mungu akamchukua kiumbe wake.
Mazishi
yantarajiwa kuwa Saa 7 mchana siku ya
Jumapili tarehen 10 Januari 2016 katika makaburi ya Njoro, Moshi Mjini, baada
ya Marehemu kuswaliwa katika Msikiti kwa Mtei ambao uko jirani na CCM kata ya
Mji Mpya Mchomba Centre.
Mwenyezi
Mungu ampumzishe amlaze
mahala
pema peponi marehemu
AMINA.
Inna
Lillahi wa inna Raji'un'
Kwa maelezo zaidi na Rambi rambi wasiliana na:
Ally Six Nurdin
au Chief Daudi Mrindoko


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...