kaimu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata
akisisitiza jambo wakati alipofanya mazungumzo na waandishi wa habari
kuhusu taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi Kushoto ni Kaimu
Kamishna wa Forodha Jocktan Kyamuhanga na kulia ni Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani Yusufu Salum .
Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi.Picha Na raymond Mushumbusi MAELEZO
Jumla ya shilingi trilioni 1.4 imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015.
Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi.Picha Na raymond Mushumbusi MAELEZO
Jumla ya shilingi trilioni 1.4 imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015.
Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la
wastani wa shilingi bilioni 490 kwa
mwezi ukulinganisha na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba
ambapo ,TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa mwezi.
Takwimu hizo zimetolewa leo jijini
Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata wakati wa
mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa taarifa kwa umma juu ya
ukusanyaji wa kodi nchini.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi kufikia Desemba mwaka huo TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi trilioni 6.4 ambayo ilikuwa ni sawa na asilimia 95.5 ya lengo la kukusanya trilioni 6.5 katika kipindi hicho.
Kaimu Kamishna huyo ametaja sababu za kuongeza kwa makusanyo ya kodi kuwa ni pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuweka mifumo mizuri ya ufuatiliaji ili kumrahisishia mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu.
Kidata amesema kuwa katika
kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano ya kuongeza mapato Mamlaka hiyo
itasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato na kuwabana wote wenye nia ya
kukwepa na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya sheria watakaobainika
wamekwepa kodi.
Katika hatua nyingine Kaimu
Kamishina Mkuu wa TRA huyo amesema jumla ya shillingi billioni 11.8zimekusanywa
kutoka kwa wafanyabiashara walioondosha makasha katika Bandari Kavu kinyume na
taratibu za forodha.
Amesema kuwa makusanyo hayo yanajumuisha shilingi bilioni 5.3 kuoka kwa Kampuni na wafanyabiashara 19 ambao wamemaliza kulipa kodi za makasha yao na wengine 19 ambao wamelipa sehemu ya kodi ya makasha yao
Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO
Dar es Salaam
6.1.2016
Sasa kwa kiasi gani Magufuli ameivusha lengo TRA? How important has the Magufuli factor been in TRA surpassing collection targets?
ReplyDeleteKwa mwendo huu elimu bure inawezekana. Hospitali dawa zitapatikana na huduma za jamii zitadumishwa. Hongera sana JPM mungu akuongezee nguvu. Pasua majibu!
ReplyDelete