Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania TRL umetangaza kusitisha kwa muda kuanzia jana Januari 01, 2016, huduma zake baada ya eneo la reli ya kati ya Kilosa mkoani  Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma tuta la reli kukumbwa na Mafuriko. 
Kwa mujibu wa taarifa za kifundi eneo lililoathiriwa na mafuriko ni kubwa hivyo Wahandisi na Mafundi  wa TRL wako eneo la mafuriko  kutathmini ukubwa wa kazi yenyewe. 
Kutokana na  uamuzi huo treni ya abiria kutoka bara ilibidi safari yake ikatizwe ilipofika Dodoma na tayari utaratibu unaandaliwa wa kupata mabasi 17 kuwasafirisaha hadi Dar es Salaam abiria 1,119 . wa treni hiyo. 
Hali kadhalika kwa vile tarahe ya kuanza tena huduma bado haijaujulikana,  safari zote kuanzia  jana Januari 01,  2016,  kwenda bara zimefutwa na abiria husika wametakiwa kufika katika vituo vya reli walikokata tiketi ili warejeshewe fedha zao na kupata fursa ya kutafuta usafiri mbadala. 
Aidha imesisitizwa kuwa Uongozi kwa wakati muafaka itatoa taarifa kamili  kuhusu lini huduma za TRL kwenda bara  zitaanza tena.
Wito unatolewa kwa kila mwananchi atakayepata taarifa hii muhimu amwaarifu mwenzake.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana.
 Dar es Salaam,
Januari 02, 2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tatizo la mafuriko eneo hili ni la kila msimu wa mvua au mvua kubwa ikinyesha. wizara husika zifanye utafiti wa kumaliza kero hii.

    Moja ya njia ya kudhibiti mafuriko eneo hili la kero ni kufanya survey ya mito ya maji na ''contours'' zinazoelekeza maji maeneo ya mafuriko ktk reli, vijiji, miji au hata ktk jiji la DSM eneo la Jangwani.

    Baada ya kubaini vyanzo vinavyo kusanya maji ya mito na ''contours'' za maeneo yanayokusanya maji yatakayosababisha mafuriko kinachofuata ni kujenga ''mabwawa'' katika maeneo ya vyanzo halisi vya mafuriko ambayo mara nyingi yapo mbali sana na reli au eneo la Jangwani DSM.

    Kwa kujenga vizuizi hivyo vya maji a.k.a mabwawa, malambo, kuta n.k vyenye milango ya kuruhusu/kuzuia mtiririko wa maji kiholela ktk vyanzo ya mafuriko basi tutaweza kuzuia mafuriko kutokea ktk maeneo ''korofi'' ya mafuriko kwa kudhibiti mtiririko wa maji kwenda maeneo ya reli n.k

    Na mwisho mabwawa , malambo, kutumiaka kama vyanzo vya matumizi ya maji na pia kumaliza tatizo ''endelevu la mafuriko kila mvua ikinyesha''

    Nakumbuka kuna mdau Dr. Sayyid PhD alitoa mada nzuri sana hapa ktk globu ya jamii kuhusu namna ya kudhibiti mafuriko wiki iliyopita, tamaa yangu ni kuwa wahusika wanasoma mawazo haya na kuyafanyia kazi.

    Mdau

    Christos Papachristou
    Diaspoara.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...