Airtel Fursa imejikita katika mradi wake wa kuwezesha vijana hapa nchini
katika ujasiliamali kupitia mpango wake wa kukomboa vijana hapa nchini wa
“Airtel Fursa Tunakuwezesha”.
Wito umetolewa kwa vijana hapa nchini kujitokeza katika kuchangamkia fursa
za kijasiriamali zinazojitokeza ili kuweza kuwaepushia vijana na matendo
maovu yanayoweza kuwafanya ndani ya jamii kukosa thamani.
Rai hiyo imetolewa na Meneja utawala VETA MVTTC Twiganile Ndunguru
Mkoani Morogoro katika warsha ya mafunzo ya Airtel fursa kwa vijana
wajasiliamali iliyo lenga kuwapatia vijana fursa katika kuendesha biashara
zao ili kuweza kujipatia kipato ambapo amesema vijana hao wanatakiwa
kijishughulisha na kuachana na mitazamo hasi huku wakipoteza muda mwingi
katika michezo isiyoweza kuleta tija katika maisha yao.
Alisema kuwa amefurahishwa sana na mpango huu wa Airtel katika kuwakomboa
vijana kwa kuwapatia mafunzo ya ujasiliamali hapa nchini kwa kuwa anaelewa
kuwa vijana wa jiji la Morogoro hususan wasichana wana muitikio mkubwa
katika swala zima la ujasiriamali na maendeleo binafsi.
Nae Meneja huduma za jamii Airtel Tanzania Hawa Bayumi amesema Airtel
Fursa pia inatoa ujuzi kwa namna gani ya kukabiliana na chagamoto ya
mfumo wa biashara ikiwemo leseni za biashara, mtaji wa kufanyia biashara
na elimu ya biashara yenye tija ambayo ndio chachu kubwa ya vijana
kushindwa kuendelea na biashara zao, huku washiriki wa mafunzo hayo
wamesema kuwa yamewnufaika kwa kiasi kikubwa kwani wameza kutambua jinsi
yakuendesha biashara zao.
Aidha alibainisha kuwa katika mchakato huu wa Airtel Fursa Tunakuwezesha,
“Airtel inatarajiwa kuwawezesha vijana wengi hapa nchini kwa kuwapatia vitendea kazi na kuweza kufikisha ndoto zao za kujikomboa kiuchumi na kuweza kujiajiri wao na kuweza kukomboa wenzao. Kwani Airtel inaamini kwamba kwa kumuwezesha kijana hapa nchini, unamuwezesha yeye mwenyewe na jamii inayomzunguka kwa kuleta maendeleo katika jamii hiyo”. Aliongeza Bayumi Warsha hiyo ilihudhuliwa na vijana zaidi ya 200 ambao wamepewa vyeti vya kushiriki ambapo mafunzo yanawahusisha watu warika mabalimbali kuanzia miaka 18 hadi 24 ambapo vijana hupatiwa mafunzo ya biashara pamoja na kupewa vitendea kazi katika kuendeleza biashara yao ili kuondokana na changamoto wanazo kabiliana nazo.

Vijana zaidi ya 200 kutoka Manispaa ya Morogoro wakiwa kwenye mafunzo na vitendea kazi kwa vijana zaidi ya 200 kupitia mradi wa Airtel Fursa yenye lengo la kuwawezesha vijana kukuza biashara na kujikwamua
kiuchuni yaliyofanyika Veta kanda ya mashariki mkoani Morogoro.

Meneja wa Utawala chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro (MVTTC), Twiganile Ndunguru akimkabidhi cheti Fabian Fredirick (25) mara baada ya kuhitimu mafunzo na vitendea kazi kwa vijana zaidi ya 200 kupitia
mradi wa Airtel Fursa yenye lengo la kuwawezesha vijana kukuza biashara na kujikwamua kiuchuni yaliyofanyika Veta kanda ya mashariki mkoani Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...